IRINGA:
Lukiza Autism Foundation ni Asasi ya Kijamii inayoshughulika na Kuelimisha Jamii kuhusu Usonji, kupigania kukubalika kwa hali ya Usonji katika jamii na ujumuishi wa watu wenye Usonji katika nyanja zote za Maisha.
Hilda Nkabe Mkurugenzi mwanzilishi wa Asasi hiyo ambaye pia ni mama mwenye mtoto mwenye usonji anasema
Mzaliwa wake wa pili mwenye umri wa miaka 16 anayeitwa Lukiza ndiye chachu ya yeye kuanzisha Asasi hiyo.
Hilda
Lukiza ni jina la Kihaya lenye maana ya UPONYAJI, Bi Hilda anasema Lengo la Asasi hiyo ni kuleta faraja katika familia zenye watoto, vijana, na watu wazima wenye usonji.
Miriamu Elisha, Mtaalamu wa Elimu Jumuishi na Mwanafunzi wa PhD Chuo Kikui Huria na Mkurugenzi wa Taasisi ya Buyegi anasema anaona wao Kama wadau wanaona ipo haja ya kuunganisha nguvu ya pamoja ili kufanikisha Lengo la uwepo wa Shule za Kati zenye mchepuo wa kiingereza Mkoani Iringa kuweza kutatua changamoto za elimu kwa watoto wenye uhitahi maalum ya kujifunza.
Ipo haja ya kuweka mazingira ya shule kuwapokea wanafunzi kulingana na uhitaji wao.
Miriamu
Miongoni mwa changamoto zinazokabili watoto wenye usonji ni pamoja na changamoto ya wataalamu wa mazoezi tiba na watambuzi wa masuala ya usonji ambapo utambuzi wa usonji hufanyika katika umri wa utoto.
Katika Taarifa ya Wizara ya Afya kupitia Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto 2021/22 – 2025/26 juu ya masuala mtambuka ya watoto Wenye ulemavu inataja uwepo wa changamoto ya upungufu wa huduma na wataalamu wa kuwasaidia watoto wenye ulemavu. sambamba na kutokuwepo nyenzo za utambuzi wa mapema katika vituo vya afya, vituo vya kulelea watoto wadogo mchana, elimu ya awali na elimu ya msingi jambo linalopelekea changamoto kubwa kwenye kuwatambua na kuwasaidia watoto wadogo
Unaweza ukatazama video hapa chini kupata taarifa kamili mwanzo mpaka mwisho.