Mkurugenzi Mtendaji wa Lukiza Autism Foundation – Hilda Nkabe akiwa na Mtoto wake Lukiza akihimiza umuhimu wa sensa ya mwaka huu na kwa nini ni muhimu zaidi kwa wazazi wenye watoto wenye ulemavu wahakikishe watoto wao wanahesabiwa.
Amehimiza pia wazazi wenye watoto wenye usonji kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuwaandikisha watoto wao.
Sensa nchini Tanzania ni tarehe 23 Agosti 2022.