PANetwork wameandaa mkutano mwisho wa mwezi huu siku ya jumamosi tarehe 27th February 2021, kuanzia saa nne asubuhi hadi saa sita mchana. (10:00am – 12:00pm)
*Agenda kuu:* Kujenga uwezo kiakili na kihisia wa wazazi wanaolea watoto wenye mahitaji maalumu.
*Mgeni Maalumu* Mr. Masoud Kipanya (mzazi wa mtoto mwenye mahitaji maalumu)
*Ajenda nyingine* zitakuwa kuhusu malezi ya watoto wenye usonji (autism) ambapo wazazi wazungumzaji watatushirikisha stori zao katika malezi.
1. Namna gani tunaweza kulea watoto katika jamii isiyoelewa kuhusu usonji (autism) kwa kujiamini – Dr. Isack Maro (Mzazi na Daktari)
2. Namna gani tunaweza kulea mtoto mwenye usonji (autism) na ndugu zake wasio na autism. – Ms. Hilda Nkabe (Mzazi na Mwanzilishi wa Lukiza Autism Foundation)
3. Kabla ya kuwaza kumpeleka mtoto shule, ni mambo yepi kama mzazi tunapaswa kuzingatia mtoto mwenye usonji (autism) kuyajua (early independence stage) – Ms. Miriam Elisha (Mzazi na Mtaalam wa Elimu)
Mkutano utafanyika kwa njia ya Zoom. Karibu mpendwa mzazi na mkaribishe na mwengine. Link hapo chini.